Bahati ya mwisho kwa wauza mihadarati

Publié le par Popote Ulipo Duniani

Serikali ya Rwanda inawashauri wale wote wanaohusika na biashara ama ulanguzi wa madawa ya kulevya kusitisha shughuli zao hizo katika msimu wa miezi sita, la sivyo watachukuliwa hatu kali mno.



Katika mahojiano na waandishi wa habari mjini Kigali, waziri wa vijana na mawasiliano Philbert Nsengimana amesema wauza mihadarati kama vile bangi wamepewa msimu wa miezi sita kuachana na biashara zao hizo zilizo haramu.

 

 

“Tunawataka wauza mihadarati kutuonyesha tu kule inakotoka, vinginevyo dini ziwaombee kwa Mwenyezi. Pia wajue bahati hiyo itakuwa na mwisho”

 

 Waziri Nsengimana ana imani kwamba harakati za kupambana na madawa ya kulevya haziwezi kuchukua muda mrefu endapo nia itakuwepo. Amesema Rwanda siyo kama nchi fulani za yAmerika Kusini( Mexico, Colombia na nyinginezo) ambapo wafanyakazi wa mihadarati na walanguzi wa mihadarati huwa wana nguvu nyingi, na wakati mwingine wakashambuliana na majeshi ya serikali kwa mapigo ya risasi.



“ Nina matumaini kwamba twaweza kutokomeza makundi hayo hata katika dakika moja endapo tukiungana nguvu”, Waziri Nsengimana ameongeza.



Biashara ya mihadarati ni mojawapo ya changamoto zinazokwaza maendeleo ya nchi. Pia ni biashara inayotajirisha kirahisi kwani hailipiwi kodi. Imeshika mizizi ndani ya Rwanda kufuatia vijana wengi kuanza kujitumbukiza katika uraibu wa kujilevya kwa sababu tofauti tofauti zikiwemo ugumu wa maisha ya nyumbani, kutokuwa na wazazi, ukosefu wa maelekezo ya wazazi hata kama bado wako hai, na hata kutangamana na marafiki wabaya.



Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa wizara inayohusika na maswala ya vijana na mawasiliano, katika kipindi hicho cha nusu mwaka serikali itapiga kampeni za kuhamasisha raia kuchunguzana wenyewe na kutoa taarifa kwa ngazi za kiraia na za usalama kuhakikisha madawa ya kulevya hayako tena.

 

Janvier NSHIMYUMUKIZA 

 

 

 

   

Publié dans Habari muhimu

Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :
Commenter cet article