Kifo cha Kanumba bado utata

Publié le par Popote Ulipo Duniani

Wapenzi wa filamu za kitanzania wanaomboleza kifo cha nguli wa filamu za bongo  Steven Kanumba ambaye ametutoka usiku kuamkia jumamosi. Kwa wale wasiomjua vizuri, Steven Kanumba ni mmojawapo ya wahusika wakuu katika filamu iitwayo OPRAH.

 

Waganga walichunguza maiti yake na kuja kuhakikisha kwamba Kanumba alikufa akiwa amelewa ndi pombe aina ya Jack Daniels, lakini mchumba wake alielezea polisi wa mkoa wa Kinondoni kuwa Kanumba alifariki wakiwa pamoja baada ya kutokea ugomvi baina yao wakiwa wawili chumbani.

 

Kama rafiki wake wa kike huyo msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu  Lulu alivyobainisha, simu yake iliita akatoka nje kwenda kuitika, Kanumba akamuuliza anani anampigia, na alipochelewa kujibiwa ndo akapandwa na hasira.

 

  Lulu alitoka nje tayari kwenda nyumbani kwake Kanumba akamrudisha nyuma alipofika kwenye get, na kumrudisha chumbani mle bidhori. Kwa mujibu wa maelezo ya Lulu, baada ya  kufunga mlango Kanumba alilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini.

Lulu na watu wote waliokuwa nyumbani kwa Kanumba, wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

 

Kanumba alikuwa akitoa mapovu mdomoni na aliwahishwa hospitali lakini muda mfupi baadae alitangazwa kuwa amefariki dunia.

Polisi wanachunguza kujua kama kweli Kanumba alilegea tu na kuanguka, ama alipigwa na kitu kizito kichwani au alisukumwa kwa nguvu na kumfanya aangukie kisogo.

 

Publié dans Makala za wasanii

Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :
Commenter cet article