Msichana wa miaka 10 ajifungua mtoto

Publié le par Popote Ulipo Duniani

Ajifungua-10.jpgMsichana mmoja wa nchini Kolombia mwenye umri wa miaka 10 tu amewashangaza watu wengi alipojifungua salama mtoto wa kike.


Cha kushangaza mno ni kwamba binti huyo ambaye amekuwa miongoni mwa wasichana wenye umri mdogo duniani kujifungua mtoto amegoma katakata kumunyonyesha mwanawe huyo.


Alipowasilishwa hospitalini akivuja damu, madaktari walilazimika kumzalisha kupitia operesheni ya upasuaji, kwa mujibu wa madaktari hao mtoto aliyezaliwa ana uzito wa kilo 2.27, yeye na mama yake wako katika hali njema kiafya ijapokuwa mtoto anaendelea kunyimwa maziwa na mama yake.


Kulingana na nifahamishe, polisi wa nchini Kolombia wametangaza mpango wao kumchukulia hatua mwanaume aliyempa ujauzito , ingawa pia sheria za Kolombia huwa zina upendeleo maalumu kwa kabila la Wayuu kuwasaidia wadumishe mila zao ambapo si jambo geni kuona wasichana kupata ujauzito wakiwa na umri mdogo.

Haijabainika wazi wazi mwanaume huyo ana miaka mingapi, kwa kuwa kuna ripoti zinazotofautiana kuhusu umri wake kama magazeti ya nchini humo yanavyoeleza, baadhi yakisema bwana huyo ana umri wa miaka 15 huku mengine yakitaja 30.

 

Janvier NSHIMYUMUKIZA

 

 

 

Publié dans Habari muhimu

Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :
Commenter cet article
A
Te teh teh, sijaaamini macho yangu. Kweli ajifungua kwa miaka kumi tu ama waliangalia ufupi wake ndio wakajiadanganya kuhusu umri wake. Mtoto wa miaka 10 huwa hajavunja ungo kwa kawaida, hii<br /> miujiza
Répondre