Atumia njia ya kikatili kumuua mkewekwa kumkalisha kwenye kiti cha umeme ili kumteketeza

Publié le par Popote Ulipo Duniani

Kiti cha umemeMwanamume mmoja nchini Uingereza ajulikanaye kama Andrew Castle alikumbwa na huzuni zilizoambatana na stress baada ya mke wake kuomba talaka ili kuivunja ndoa yao

 

Andrew Castle mwenye umri wa miaka 61  hakuweza kuvumilia kuona ndoa yao inavunjika kiasi cha kwamba aliandaa mpango wa kumuua mkewe kwa kumkalisha kwenye kiti cha umeme.

Andrew alikiandaa kiti cha chuma alichokiunganisha na umeme na kisha alimuomba mkewe akae kwenye kiti hicho.

 

 

 

Kiti Cha Umeme

Huku akitegemea mkewe angekaa kwenye kiti hicho ili aweze kuwasha umeme, mkewe kwa bahati nzuri bila kujua alienda kukaa sehemu nyingine.

Baada ya kuona mpango wake haujaenda kama alivyopanga, Andrew alianza kumtandika virungu mkewe aliyetajwa kwa jina la Margaret ambaye naye pia ana umri wa miaka 61.

Kwa mujibu wa nifahamishe, Margaret alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia nje ya nyumba yao ambapo ugomvi wao uliendelea kabla ya majirani hawajaingilia kati kuwatenganisha na kisha kuwaita polisi.

  Janvier Nshimyumukiza

  

Publié dans Habari muhimu

Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :
Commenter cet article