Sudan Kusini yajitangazia uhuru wake na kuwa taifa jipya kuzaliwa duniani
Sudan Kusini imejitenga na Kaskazini na kutangaza rasmi uhuru wake na kuwa taifa jipya kuzaliwa duniani.
Nchi mpya ya Sudan Kusini ambayo Mji wake mkuu ni Juba, itakuwa na utajiri wa mafuta lakini itakuwa moja ya nchi maskini kabisa duniani kutokana na mapigano yaliyoikumba kwa muda mrefu. mapigano hayo yalipelekea watoto kutopata nafasi ya kujifunza kiasi kwamba watoto chini ya miaka 13 hawasomi huku pia 84% ya wanawake hawajui kusoma na kuandika
Sehemu iliyopigwa rangi
nyekundu ndiyo Sudan Kusini
Ijapokuwa Sudan Kusin imejitenga na kaskazini, Uraia ni suala ambalo bado lipo na utata. Redio ya Taifa Sudan imeripoti kuwa uraia wa Wasudan Kusini wanaoishi kaskazini umekwishafutwa, na maelfu ya wafanyakazi Wasudani Kusini wanaofanya kazi kaskazini walilazamika kuacha kazi zao kabla ya kugawanyika.
Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba Kaskazini na Kusini hazijaamua maeneo ya Abyei na Kordofan yenye utajiri wa mafuta yatachukuliwa na taifa gani.
Janvier Nshimyumukiza