Sudan: Chumba cha kuulia wapinzani wa Bashir chabainika, chabatizwa jina la White House
Wakati wakazi wa Sudan wakishughulika kama nyuki kuamua iwapo Sudan Kusini itajitenga na Sudan Kaskazini na kujitawala kama taifa huru au la, kumebainika chumba kilichokuwa kinatumika kusimangia na kuulia wapinzani wa Rais wa nchi hiyo , Omar El Bashir.
White House mpya
BBC iliripoti kuwa mwandishi wake amewahi kutinga chumbani humo ambamo umati mkubwa wa wapinzani wa Omar Bashir na wengine waliodaiwa kuwapa uungaji mkono wao wamekuwa wakisimangwa na wakiuliwa kama nzi, wote wakiwa ni kutoka Sudan Kusini
Chumba hicho kilichoko Juba, jijini mwa Sudan kusini , kimebatizwa jina sawa na lile la ikulu ya Jamhuri za Kimarekani, white House.
Mwandishi huyo wa BBC amesema kuwa kwa macho yake mwenyewe aliona mapingu yakining'inia paa la chumba hicho na mabaki ya risasi sakafuni.
Idadi kamili ya watu waliopoteza maisha yao ndani ya White House haijajulikana, ila afisa mkuu mmoja wa majeshi ya Sudan Kusini alkadiria kuwa watu hao wanafikia maelfu.
BBC Gahuza
Janvier Nshimyumukiza