Hayati Nibishaka Aimable azikwa

Publié le par Popote Ulipo Duniani

nibishaka-aimable.jpg

Ijumaa iliyopita mamia ya watu wakiwemo jamaa, marafiki walikuwa wamefurika kwenye majengo ya Bunge hapo Kimihurura kumuaga na kumsindikiza hadi kwenye maziara Marehemu Nibishaka Aimable, ambaye alifariki siku ya jumatatu,  julai 4 mwaka huu.

 

Ujumbe wa kuomboleza wa  rais Paul Kagame uliotolewa kwa bunge na waziri Protais Musoni , ulielezea kuwa hayati Nibishaka kiukweli alikuwa mzalendo  na shujaa, na  alitumikia taifa lake ipasavyo.

 

 

 

 Hayati Nibishaka Aimable

Ushujaa wa marehemu na utashi wake kulitumikia taifa lake uligusiwa hata na katibu mkuu wa RPF Inkotanyi, Francois Ngarambe katika hotuba yake ambapo alisema kuwa hayati alifariki wakati akihitajika zaidi.


  Bwana Ngarambe aliongeza kuwa hayati Nibishaka  alitumia bidii na jitihada kulitumikia taifa lake tangu wakati wa vita vya kujikomboa vilivyoingiza madarakani chama chake cha RPF.

Mwenyekiti wa baraza la seneti Dr. Vincent Biruta alidokeza kuwa Aimable Nibishaka aliacha pengo lisiloweza kujazwa na mtu yeyote yule, hivyo akaisihi familia yake kupiga moyo konde kukabiliana na hali ya maisha.

Nibishaka Aimable alizaliwa julai 7, 1942 wilayani Burera.

 

Aliaga dunia jumatatu tarehe 4 julai na kuzikwa jana alasiri.

 

 

Nshimyumukiza Janvier

 

Publié dans Habari muhimu

Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :
Commenter cet article