Wawili wafikishwa mahakamani kuhusiana na kifo cha Jean Leonard Rugambage

Publié le par Popote Ulipo Duniani

Rugambage.jpgJana  wamewasilishwa mahakamani watu wawili wanaoshikiliwa kwa madai kwamba wanahusiana na kifo cha Jean Leonard Rugambage alias sheriff ambaye alikuwa mhariri msaidizi wa gazeti la Umuvugizi.

 

Washukiwa hao ni pamoja na Nduguyangu Didace aliyewahi kuwa mwanajeshi, na Karemera Antoine aliyekuwa afisa wa polisi. 

 

 

Marehemu Jean Leonard rugambage

 

Nduguyangu  alikubali hatia na  kuomba awiwe radhi kwa vile alivyokubali hatia kwa hatua ya kwanza, huku mwenzake alikataa katakata kuhusiana na kifo hicho kwa njia yoyote ile.

Nduguyangu Didace alikiri kumfyatulia risasi hayati Rugambage Jean Leonard kwa kutumia bunduki ndogo ya aina ya bastola ijapokuwa hakuwa anamjua, bali aliongeza alihusika na umwagaji damu huo kutekelezea mpango aliopewa  na askari-polisi Karemera Antoine.

Karemera alisema kuwa mahakama hupuuzia na kuvaalia miwani kujitetea kwake na jinsi asivyohusika katu na kifo cha Rugambage, hivyo akaomba mahakama imtakase na hatia inayomkabili. 

Mwendeshaji wa mashtaka aliziona hatia kuwa kali mno kiasi cha kuombea washukiwa wote wawili kifungo cha maisha jela, ila mahakama ilisema itasoma hukumu tarehe 16 septemba  mwaka huu.

Leonard Rugambage alifyatuliwa risasi na kufariki dunia papo hapo alipovamiwa karibu na nyumba yake tarehe 24 juni mwaka jana.

 

 

Janvier Nshimyumukiza

 

Publié dans Habari muhimu

Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :
Commenter cet article